HAT-TRICK YA KANE YAIPELEKA TOTTENHAM NAFASI YA PILI EPL.

Tokeo la picha la kane hattrick image

EPL, Ligi Kuu England, imerejea jana baada kukosekana tangu Januari 4 kwa Mechi ya mapema huko White Hart Lane Jijini London na Wenyeji Tottenham Hotspur kuifunga West Bromwich Albion 4-0.
 
Ushindi huu wa Spurs umewaweka Nafasi ya Pili kwenye EPL wakiwa Pointi 4 nyuma ya Vinara Chelsea ambao ndio waliwafunga hapo hapo White Hart Lane 2-0 kwenye Mechi yao ya mwisho Januari 4.

 Tokeo la picha la kane hattrick image
 
Spurs waliweka Bao lao la kwanza Dakika ya 12 baada Pasi ya Christian Eriksen kumkuta Harry Kane na kufunga. Bao la Pili la Spurs lilifungwa Dakika ya 26 kufuatia Shuti la Christian Eriksen kumgonga Mchezaji wa WBA Jonas Olsson na kisha mwenzake Gareth McAuley na kutinga.
 
Hadi Haftaimu Spurs 2 WBA 0.
Kipindi cha Pili Harry Kane alikamilisha Hatitriki yake kwa kufunga Bao 2 Dakika za 77 na 82 na kuiweka Spurs 4-0 mbele.

Jumapili hii kuna Mechi 2 ikianza ile ya Goodison Park kati ya Everton, walio Nafasi ya 7, na Man City ambao wako Nafasi ya 4. Hapo baadae utafuata mtanange huko Old Trafford wakati Man United ambao wapo kwenye wimbi la kushinda Mechi 9 mfululizo wakicheza na Mahasimu wao wa Jadi Liverpool.
 
Wimbi hili la ushindi kwa Man United ni refu tangu Msimu wa 2008/09 waliposhinda Mechi 11 mfululizo kati ya Januari na Februari na kuelekea kutwaa Ubingwa wa England na Kombe la Ligi wakiwa chini ya Meneja Lejendari Sir Alex Ferguson.
 
VIKOSI VILIVYOANZA:
 
TOTTENHAM HOTSPUR (Mfumo 3-4-2-1): Lloris; Dier, Alderweireld, Vertonghen; Walker, Wanyama, Dembele, Rose; Eriksen, Dele; Kane
Akiba: Vorm, Trippier, Davies, Nkoudou, Sissoko, Winks, Son
 
WEST BROM (Mfumo 4-2-3-1): Foster; Dawson, McAuley, Olsson, Brunt; Fletcher, Yacob; Chadli, Morrison, Phillips; Rondon
Akiba: Myhill, Galloway, Leko, McClean, Field, Robson-Kanu, Wilson
Tokeo la picha la Anthony Taylor IMAGE
Anthony Taylor
 
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment