VINARA
wa EPL, Ligi Kuu England, Chelsea, Jana wamezidi kujizatiti kileleni
baada ya kuichapa Hull City 2-0 huko Stamford Bridge.
Ushindi huu umeiweka Chelsea kuwa Pointi 8 mbele ya Timu ya Pili Arsenal.
Bao za ushindi wa Chelsea zilifungwa na Diego Costa na Garry Cahill katika Dakika za 52 ya Kipindi cha Kwanza na 81.
Kipindi
cha Kwanza cha Mechi hii kilirefushwa kwa Dakika 7 baada ya kusimama
kumtibu Majeruhi Mason wa Hull City kwenye Dakika ya 21.
Mechi inayofuata kwa Chelsea ni Ugenini huko Anfield hapo Jumanne Januari 31.
VIKOSI:
Chelsea (Mfumo 3-4-3): Courtois; Azpilicueta, David Luiz, Cahill; Moses, Kante, Matic, Alonso; Pedro, Diego Costa, Hazard.
Akiba: Begovic, Ake, Zouma, Chalobah, Fabregas, Willian, Batshuayi.
Hull (Mfumo 3-5-1-1): Jakupovic; Maguire, Dawson, Davies; Elabdellaoui, Mason, Huddlestone, Clucas, Robertson; Evandro; Hernandez.
Akiba: Marshall, Meyler, Diomande, Maloney, Niasse, Tymon, Bowen.
| Neil Swarbrick. |
0 Maoni:
Post a Comment