Arsenal
wakiwa kwao Emirates wamefanikiwa kushinda 2-1 kwa Penati Dakika za
Majeruhi wakati wakiwa Mtu 10 na pia kumpoteza Meneja wao Arsene Wenger
alietolewa nje ya Uwanja na Refa.
Ushindi
huo umewaweka Arsenal Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 9 nyuma ya Vinara
Chelsea.
Arsenal
walitangulia kufunga Dakika ya 59 kwa Bao la Sentahafu wao Mustafi
lakini Dakika ya 65 wakabaki Mtu 10 baada Kiungo wao Xhaka kupewa Kadi
Nyekundu.
Burnley
walisawazisha kwa Penati ya Dakika za Majeruhi zilizoongezwa 7 kupitia
Gray katika Dakika ya 93 baada ya Refa Jon Moss kuamua Francis Coquelin
alimchezea Faulo Ashley Barnes na Andre Gray kusawazisha.
Tukio hilo lilimfanya Wenger alalamike sana na Refa Moss kumtimua Uwanjani.
Lakini
Refa huyo, katika Dakika ya 98, aliwapa Arsenal Penati baada kuamua
Buti ya Ben Mee ilikuwa juu Kichani mwa Laurent Koscielny na Alexis
Sanchez kufunga Bao la Pili na la ushindi kwa Arsenal.
Mapema Jana, Southampton wakiwa kwao Saint Mary, waliwatandika Mabingwa
Watetezi Leicester City 3-0 kwa Bao za Ward-Prowse, Rodriguez na Penati
ya Tadic na kuwaacha Mabingwa hao wakiwa wameenda Gemu 11 za Ugenini
kwenye EPL Msimu huu bila ushindi.
Sasa Leicester wapo Nafasi 3 juu ya zile Timu 3 za mkiani huku Southampton wakipanda hadi Nafasi ya 11.
Ligi Kuu England Ratiba
++Saa za Bongo++
[Zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku isipokuwa inapotajwa]
Jumanne Januari 31
Arsenal v Watford
Bournemouth v Crystal Palace
Burnley v Leicester City
Middlesbrough v West Bromwich Albion
Sunderland v Tottenham Hotspur
Swansea City v Southampton
2300 Liverpool v Chelsea
Jumatano Februari 1
West Ham United v Manchester City
2300 Manchester United v Hull City
2300 Stoke City v Everton
Jumamosi Februari 4
1530 Chelsea v Arsenal
1800 Crystal Palace v Sunderland
1800 Everton v Bournemouth
1800 Hull City v Liverpool
1800 Southampton v West Ham United
1800 Watford v Burnley
1800 West Bromwich Albion v Stoke City
2030 Tottenham Hotspur v Middlesbrough
Jumapili Februari 5
1630 Manchester City v Swansea City
1900 Leicester City v Manchester United
0 Maoni:
Post a Comment