Sir Bobby Charlton, ambae kwa muda mrefu alishikilia Rekodi ya
kufunga Bao nyingi Klabuni Manchester United hadi Juzi ilipovunjwa na
Wayne Rooney, amemsifia Straika huyo na kumsema ni 'Lejendari wa kweli
kwa Klabu na Nchi yake'.
Wakiwa nyuma kwa Bao 1-0 walipocheza na Stoke City Ugenini kwenye
Mechi ya EPL, Ligi Kuu England, Rooney aliisawazishia Man United kwa
Frikiki ya Dakika ya 94 na kufikisha Bao 250 akiivunja Rekodi ya Sir
Bobby Charlton aliefunga Bao 249 iliyodumu kwa Miaka 44.
Sir Bobby Charlton alikuwepo kwenye Mechi hiyo ambapo mwishoni alikwenda Vyumba vya Kubadili Jezi kumpongeza Rooney.
Akiongea baadae, Sir Bobby alisema: "Nitakuwa mwongo nikisema
sikuhuzunika kuipoteza hii rekodi. Lakini ukweli nimefurahishwa na
Wayne. Anastahili mahala kwenye Vitabu vya Historia. Yeye ni Lejendari
wa kweli wa Klabu na Nchi yake na ni sahihi yeye kuwa ndie Mfungaji Bora
kwa Man United na England!"
Nae Sir Alex Ferguson, aliekuwa Meneja wa Man United kuanzia 1986
hadi 2013 na Agosti 2004 kumnunua Rooney kutoka Everton, amesema: "Nampa
pongezi kubwa Wayne kwa rekodi hii. Wayne anastahili kuwemo kwenye
Historia wa Klabu hii kubwa na nina hakika atafunga Bao nyingi zaidi.
Meneja wa sasa wa Man United, Jose Mourinho, ameeleza:: "Ni rekodi
ya Klabu kubwa kabisa England na moja ya Klabu kubwa Duniani. Kabla ya
hapo rekodi hiyo ilishikiliwa na Lejendari wa Klabu. Sasa Wayne anakuwa
Lejendari wa Manchester United."
Rooney, mwenye Miaka 31, amesema: "Naskia fahari sana. Hakikuwa ni
kitu nilichokitegemea nilipojiunga! Wachezaji wanaochezea Klabu hii ni
kiwango cha Dunia. Nasikia fahari kuichezea Klabu hii na kuwa ndie
Mfungaji Bora katika Historia yake ni tuzo kubwa mno!"
Nae Meneja wa England Gareth Southgate, akiongea na Tovuti ya FA,
Chama cha Soka England, ametamka: "Ukiangalia ni Rekodi ya nani
ameivunja na jinsi ambavyo Sir Bobby anavyopendwa na Nchi na Klabu yake
inaonyesha wazi hii ni sifa kubwa. Kuwa Mfungaji Bora kwa Man United na
pia England ni mafanikio makubwa mno! Kufunga Bao zote hizo kunataka uwe
Mchezaji mzuri kwa kipindi kirefu!"
0 Maoni:
Post a Comment