Meneja wa Leicester City Claudio
Ranieri amesema anataka sana Mwitaliano mwenzake Antonio Conte ashinde
Ligi ya Premia na viongozi wa ligi wa sasa Chelsea.
Ranieri, 65, aliiongoza Leicester kushinda ligi msimu uliopita kwa njia ya kushangaza.
Lakini kwa sasa Leicester wamo nambari 15 ligini, alama 34 nyuma ya klabu hiyo yake ya zamani.
"Kama mkufunzi wa zamani wa Chelsea na shabiki wa Italia, natumai Conte atatimiza lengo hilo," Ranieri amesema.
"Ameonesha kwamba makocha wa Italia ni stadi sana."
Ranieri
ana mkataba Leicester hadi 2020 lakini anakubali kwamba nafasi yake
katika klabu hiyo haiko salama, licha ya kufikia ufanisi wa kushangaza
msimu uliopita.
"Natumai nitasalia England," aliongeza.
"Ninahisi
vyema hapa, ingawa katika kandanda mnakuwa juu kwenye nyota leo na
kesho yake mnajipata chini sakafuni, kwa hivyo usiwahi kudhania.
0 Maoni:
Post a Comment