Aristica Cioaba |
Kocha
mpya wa Azam FC, Mromania, Aristica Cioaba, kwa mara ya kwanza Jumamosi
ijayo anatarajiwa kukaa katika benchi kuiongoza timu hiyo
itakapopambana na Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa
Uwanja wa Uhuru, Dar.
Mromania
huyo ambaye amepewa mkataba wa miezi sita na Azam akichukua nafasi ya
Mhispania, Zeben Hernandez aliyetimuliwa mwishoni mwa mwaka jana, bado
hajaanza kazi rasmi ya kuinoa timu hiyo kutokana na kukosa kibali cha
kufanyia kazi hapa nchini.
Meneja
wa timu hiyo, Philip Alando, amesema: “Kila kitu tumekamilisha kwa
maana ya kulipia gharama za kupata kibali, kilichobaki kwa sasa ni
kusubiri tu uhamiaji kuona ni lini watatupatia hicho kibali.
“Kwanza
tumeomba kibali cha kazi, tutakapokipata, ndipo tutafanya mchakato wa
kuomba kibali cha makazi, matarajio yetu ni kuona kabla hatujapambana na
Simba tumekamilisha kila kitu ili kocha wetu huyu aanze rasmi kazi.”
Ikumbukwe
kuwa, kwa sasa kikosi cha Azam kinanolewa na kocha wa muda, Idd Nassor
Cheche baada ya Zeben na benchi lake la ufundi lililokuwa likiundwa na
Wahispania watano kufutwa kazi kutokana na matokeo mabaya waliyokuwa
wakiyapata.
0 Maoni:
Post a Comment