EPL KUSIMAMA KUZIPISHA EFL CUP NA FA CUP KUENDELEA.

 Picha inayohusiana
WAPENZI wa EPL, Ligi Kuu England, watapaswa kusubiri hadi Januari 31 ili kupisha Nusu Fainali za Kombe la Ligi, EFL, CUP, ambazo zitachezwa Jumatano na Alhamisi hii na kisha kuanzia Ijumaa hadi Jumapili patakuwepo na Mechi za Raundi ya 4 ya EMIRATES FA CUP.
 
EPL itakuwepo angani Jumanne Januari 31 kwa Mechi 7 na Jumatano Februari Mosi zipo Mechi 3 lakini Jumanne ndio ipo Bigi Mechi huko Anfield kati ya Liverpool na Chelsea.

PATA RATIBA ZA EFL CUP, FA CUP na EPL:
EFL CUP.
 
Kwa vile Nusu Fainali hizi huchezwa kwa Mikondo Miwili ya Nyumbani na Ugenini na kwa vile Mechi zake za kwanza zimeshachezwa, hivyo Marudiano ya Mechi hizi yatakuwa hapo Januari 25 na 26 huko Anfield na KCOM Stadium.
Katika Mechi za Kwanza Man United iliifunga Hull City 2-0 huko Old Trafford na Liverpool kufungwa 1-0 huko Saint Mary na Southampton.
@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@
JE WAJUA?
-Msimu huu hili Kombe la Ligi halina Mdhamini na limebatizwa English Football League Cup, EFL CUP.

-Huko nyuma Kombe la Ligi, kwa sababu za kiudhamini, liliwahi kubatizwa Coca-Cola Cup, Worthington Cup, Carling Cup na Capital One Cup.
@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@
 
EFL CUP
Nusu Fainali
MARUDIANO
**Saa za Bongo
**Kwenye Mabano Mabao Mechi ya Kwanza
 
Jumatano Januari 25
2300 Liverpool v Southampton [0-1]
 
Alhamisi Januari 26
2245 Hull City v Manchester United [0-2]

 @@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@

EMIRATES FA CUP – Raundi ya 4
Mechi za Raundi ya 4 ya FA CUP zitaanza Ijumaa Januari 27 kwa Mechi moja tu kati ya Derby County na Mabingwa wa England Leicester City.
Siku ya pili zipo Mechi 10.
Mabingwa Watetezi wa FA CUP, Manchester United wao watacheza Raundi ya 4 kwao Old Trafford na Wigan Athletic hapo Jumapili Januari 29.
@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@
 
JE WAJUA?
  • FA CUP 2016/17, ambalo pia hujulikana kama FA Challenge Cup, ni mara ya 136 kushindaniwa kila Mwaka tangu lilipoanzishwe na linatambuliwa kama ndio Mashindano ya kale kupita yote Duniani.
  • Kombe hili linadhaminiwa na Kampuni ya Ndege ya Emirates na kwa sababu za kiudhamini linaitwa Emirates FA Cup.
  • Timu 736 zilikubaliwa kushiriki Mashindano haya Msimu huu na yalianza kwa Raundi ya Awali na yatafikia Tamati kwa Fainali itakayochezwa Uwanjani Wembley Jijini London hapo Mei 27, 2017.
  • Mshindi wa FA CUP ataingizwa Hatua ya Makundi ya UEFA EUROPA LIGI Msimu wa 2017/18.
  • Bingwa Mtetezi ni Manchester United.
@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@
 
EMIRATES FA CUP:
RAUNDI YA 4
**Saa za Bongo
Ijumaa Januari 27
2255 Derby County v Leicester City     
           
Jumamosi Januari 28
1530 Liverpool v Wolverhampton Wanderers              

1800 Blackburn Rovers v Blackpool       
1800 Chelsea v Brentford           
1800 Middlesbrough v Accrington Stanley       
1800 Oxford United v Newcastle                 
1800 Rochdale v Huddersfield Town               
1800 Lincoln City v Brighton & Hove Albion                 
1800 Burnley v Bristol City               
1800 Tottenham Hotspur v Wycombe Wanderers                 
2030 Southampton v Arsenal       
   
Jumapili Januari 29
1500 Millwall v Watford             

1530 Fulham v Hull City            
1700 Sutton United v Leeds United                 
1900 Manchester United v Wigan Athletic      
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment