ARSENE WENGER APELEKWA KWA PILATO WA FA.

 Tokeo la picha la WENGER IMAGE YA KUMSUKUMA REFA

FA, Chama cha Soka England, kimemfungulia rasmi Mashitaka ya Utovu wa Nidhamu Meneja wa Arsenal Arsene Wenger kwa madai ya kumkashifu Refa na pia kumsukuma Refa wa Akiba.
 
Jumapili, kwenye Mechi ambayo Arsenal iliifunga Burnley 2-1, Wenger alimsukuma Refa wa Akiba Anthony Taylor mara tu baada ya kuamriwa na Refa wa Mechi hiyo Jon Moss kutoka nje ya Uwanja kwa kumkashifu ikidaiwa alimwita ‘laghai’.

Wenger alitupwa nje ya Uwanja Dakika ya 93 mara baada ya Burnley kupewa Penati ambayo walisawazisha Bao na Gemu kuwa 1-1 lakini Dakika chache baadae Refa huyo huyo, Jon Moss, aliekuwa mbaya ndie aliwapa Arsenal Penati tata na kufunga Bao lao la ushindi katika Dakika ya 98.

Mara baada ya Mechi hiyo, Wenger, mwenye Miaka 67, aliungama na kuomba radhi.

Lakini Leo, FA imetoa tamko rasmi la kumfungulia Mashitaka ya Utovu wa Nidhamu na kumpa hadi Alhamisi Saa 3 Usiku, Saa za Bongo, kujibu Mashitaka yake.

Mwaka 2012, Meneja wa Newcastle wakati huo, Alan Pardew, alitwangwa Faini Pauni 20,000 na kufungiwa Mechi 2 kwa kumsukuma Refa Msaidizi, Mshika Kibendera.

Lakini, hii Leo, Marefa Wastaafu wa England, akiwemo Keith Hackett na Howard Webb, wamekuja juu na kutaka itolewe Adhabu kali kwa Wenger kwa Kifungo kisichopungua Mechi 6 ili kuwa Onyo kali kwamba Marefa hawaguswi.


Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment