MECHI
za Kundi B la AFCON 2017, Mashindano ya 31 ya Fainali za Kombe la
Mataifa ya Afrika, zimekamilika Jana huko Gabon kwa Tunisia kuungana na
Senegal iliyofuzu mapema huko Robo Fainali.
Jana,
Senegal, wakicheza kukamilisha Ratiba tu kwani walishatinga Robo
Fainali wakiwa na Mechi mkononi, walitoka Sare ya 2-2 na Algeria wakati
Tunisia ikiichapa 4-2 Zimbabwe ambayo ilikuwa ishatupwa nje kabla ya
Mechi hiyo.
Bao
za Senegal hiyo Jana zilifungwa na Papakouly Dipo na Moussa Sow Dakika
za 43 na 53 wakati za Algeria zikipigwa na Islam Slimani Dakika za 10 na
52.
Katika
Mechi ya Pili ya Kundi B, Tunisia iliichapa Zimbabwe 4-2 na kufuzu Robo
Fainali wakiwa nyuma ya Washindi wa Kundi B Senegal.
Mabao
ya Mechi hiyo yalifungwa na Musona, Dakika ya 42 na Ndoro, 58, kwa
upande wa Zimbabwe na Sliti, Dakika ya 9, Msakni, 22, Khenissi, 36, na
Penati ya Khazri, 45.
Kwenye Robo Fainali, Senegal itacheza na Cameroon na Tunisia kuivaa Burkina Fasso.
Leo
zipo Mechi za mwisho za Kundi C kati ya Morocco na Ivory Coast na
nyingine ni katii ya Togo na Congo DR huku Wawili wowote kati yao wakiwa
na nafasi ya kufuzu.
0 Maoni:
Post a Comment