HUKU West Ham ikipiga chini Ofa ya 3 ya Klabu ya France Marseille
kumnunua Dimitri Payet kutoka West Ham, Everton imeruhusu Winga wao
Gerard Deulofeu kujiunga na AC Milan ya Italy kwa Mkopo.
PAYET:
West Ham imeikataa Ofa ya 3 kutoka kwa Marseille ya France ya kumnunua Mchezaji wa France Dimitri Payet.
Inaaminika Dau la sasa lililowekwa Mezani ni Pauni Milioni 22.5.
Mwenyewe Payet anang'ang'ania kuondoka arejee Marseille akitaja
sababu za Kifamilia lakini West Ham wamegoma na kudai hawana shida ya
Fedha kwa kumuuza ingawa wanamthamini kuwa Dau lake ni Pauni Milioni 30.
West Ham walimnunua Payet, mwenye Miaka 29, kwa Pauni Milioni 10.75
mwanzoni mwa Msimu wa 2015 na Februari Mwaka Jana alisaini Mkataba mpya
mrefu na West Ham baada kuwa ndie Mchezaji Bora wao kwa Msimu uliopita.
Tangu mzozo huo uibuke, Payet hajacheza Mechi 2 za Ligi lakini zote West Ham wameshinda.
GERARD DEULOFEU:
WINGA wa Everton Gerard Deulofeu mwenye Miaka 22 atajiunga na AC Milan ya Italy kwa Mkopo.
Msimu huu Deulofeu ameichezea Everton Mechi 13 na Meneja wa Timu
hiyo Ronald Koeman amesema wamemruhusu kuondoka ili apate muda mwingi wa
kucheza Mechi.
Deulofeu, Raia wa Spain, alijiunga na Everton kwa Mkopo Msimu wa
2013/14 kutoka Barcelona na Mwaka 2015 kununuliwa moja kwa moja kwa
Pauni Milioni 4.3.
0 Maoni:
Post a Comment