Kiungo wa kati wa Manchester City
Yaya Toure amesema winga wa klabu hiyo Raheem Sterling alifaa
kujiangusha na kuishindia klabu yake penalti wakati wa mechi yao dhidi
ya Tottenham Hotspur Jumamosi.
Mechi hiyo ilimalizika kwa sare ya 2-2.
City walikuwa wanaongoza 2-1 pale Sterling alipopata mwanya wa kushambulia eneo la hatari.
Hata hivyo, alisukumwa na beki wa Spurs Kyle Walker ingawa hilo halikuonekana na mwamuzi wa mechi Andre Marriner.
Baada ya mechi, Walker alikiri "Sikuwa naenda kuufikia mpira."
Toure amesema: "Ukiwa na uzoefu kama wangu, labda unaweza kujiangusha."
Muda mfupi baada ya mfarakano kati ya Walker na Sterling, Tottenham walisawazisha kupitia Son Heung-min.
Sare hiyo iliwafanya City, ambao walikuwa wameongoza 2-0 wakati mmoja, kusalia nambari tano kwenye jedwali.
"Hizo ni alama mbili zinapotea," Toure aliongeza.
"Tottenham ani wazuri. Wanacheza vyema sana, wana nguvu, wanapigania mipira, lakini tulistahiki alama hizo tatu."
Kuhusu
kisa cha Sterling, Toure alisema: "Alikuwa mkweli sana, anataka kutenda
haki wakati wa mechi kama hizi. Iwapo kijana huyo ni mtu wa aina hiyo,
huwezi kumwambia alikosa.
"Unapotazama, hangekosa kufunga - lakini Walker alimsukuma kutoka nyuma.
"Mwamuzi
akitazama video baada ya mechi, atahisi haki haikutendeka. Sote hutenda
makosa maishani, lakini hili ni chungu kulikubali."
0 Maoni:
Post a Comment