MABINGWA
Watetezi wa Kombe la Mfalme wa huko Spain, Copa del Rey, FC Barcelona,
Jana waliitandika Real Sociedad Bao 5-2 kwenye Mechi ya Pili ya Robo
Fainali.
Kwenye
Mechi ya Kwanza iliyochezwa huko Anoeta Stadium, Barca ilishinda 1-0 na
hivyo sasa wametinga Nusu Fainali kwa Jumla ya Mabao 6-2.
Hapo Jana, Bao za Barca zilifungwa na Denis Suarez, Bao 2, Lionel Messi, Penati, Luis Suarez na Arda Turan.
Bao za Real Sociedad zilipachikwa na Juanmi na Da Silva.
Kwenye Nusu Fainali, Barcelona, ambao wametwaa Copa Del Rey mara 28, wataungana na Atletico Madrid, Celta Vigo na Alaves.
Droo ya Nusu Fainali itafanyika baadae Leo
0 Maoni:
Post a Comment