Leo naomba tuhame kidogo kwenye soka na tuangalie mpira wa kikapu kidogo ambapo kiungomshambuliaji inakuletea habari hii;
Mchezaji wa mpira wa kikapu nchini
New Zealand Akil Mitchell amesema anapata nafuu baada ya jicho lake
kutoka alipokuwa uwanjani akicheza.
Mitchell huchezea klabu ya New
Zealand Breakers, na alikuwa mjini Auckland kucheza mechi ya NBL ya
Australia Alhamisi usiku kisa hicho kilipotokea.
Mchezaji wa timu pinzani aliingiza kimakosa kidole ndani ya tundu la kishimo cha jicho na ghafla jicho lake likatoka nje.
Mchezaji
huyo mzaliwa wa Marekani alianguka sakafuni akiwa ametumia mikono yake
kufunika jicho lake la kushoto na akakimbizwa hospitalini.
"Kwa viganja vya mkono wangu, nilihisi mboni ya jicho ikiwa nje
na kukaa upande mmoja wa uso," aliambia Radio Sport ya New Zealand.
"Bado jicho hilo lilikuwa linaona."
"Nakumbuka
nikifikiria, bwana we ... hii ni hali mbaya, lakini nilihisi kwamba
lilikuwa jambo la kushangaza na hapo ndipo niliingiwa na wasiwasi
kiasi."
Mchezaji huyo wa miaka 24 anasema anakumbuka kusikia mashabiki na wachezaji wake wakiingiwa na wasiwasi.
Alidhani hangeweza kuona tena na kwamba uchezaji wake ulikuwa umefikia kikomo.
"Nilipoingizwa
kwenye gari la kubeba wagonjwa walinipa dawa za kupunguza maumivu na
matoneo kadha ya dawa yenye chumvi machoni na nikasakia mboni ya jicho
ikirudi ndani, jambo ambalo pia lilikuwa la ajabu."
"Najihisi mwenye furaha sana kuweza kufunga na kufungua macho tena, ni jambo la kushangaza."
Baada
ya kuruhusiwa kuondoka hospitalini Alhamisi, aliandika kwenye Twitter
kwamba "najihisi vyema" na akatumia picha za vibonzo maarufu kama emoji
za mboni za jicho.
Mchezaji huyo kutoka jimbo la North Carolina,
Marekani anatarajiwa kupona kabisa na huenda akarejea uwanjani kucheza
hivi karibuni.
0 Maoni:
Post a Comment