FEDHA ZA CHINA ZAMKOSESHA DIEGO COSTA MECHI DHIDI YA MABINGWA LEICESTER CITY!

Tokeo la picha la DIEGO COSTA IMAGE

TRAIKA Diego Costa ametupwa nje ya Kikosi cha Chelsea ambacho Leo kipo huko King Power Stadium kucheza na Mabingwa Watetezi Leicester City katika Mechi ya EPL, Ligi Kuu England.
 
Habari za ndani zimedai upo mzozo wa Costa, mwenye Miaka 28, na uongozi wa Klabu akisindikiza ahamie China kwa Dau la Pauni Milioni 30.

Hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la Wachezaji Wakubwa Duniani kutua huko China ambako wanalipwa Mishahara minono mno.

Wiki yote hii, Costa amekuwa hayupo Mazoezini akidai ameumia na pia kuzozana na Madktari wa Viungo wa Chelsea mzozo ambao umesemekana ulimhusisha pia Meneja Antonio Conte.

Hivi sasa ripoti zimedai Wakala wa Conte, Jorge Mendes, yupo huko China. Kikosi cha Chelsea ambacho Jana kilijumuika pamoja kuelekea huko Leicester kiliondoka bila Costa.

Hata hivyo, msimamo wa Chelsea ni kwamba hawatamuuza Mchezaji huyo Mzaliwa wa Brazil anaechezea Spain na watabaki nae hadi mwisho wa Mkataba wake hapo 2019.

Msimu huu, Costa ameifungia Chelsea Bao 14 na kuasisti mara 5 huku Chelsea ikiongoza EPL ikiwa Pointi 5 juu kileleni mbele ya Timu ya Pili Liverpool.

Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment