
VINARA
wa La Liga huko Spain Real Madrid Jumapili watakuwa Wenyeji wa Timu
ngumu Real Sociedad na sasa wapo kwenye kibarua kigumu cha kugeuza fomu
yao iliyoporomoka ambayo imewafanya washindwe kushinda katika Mechi zao 3
kati ya 4 zilizopita.
Katikati ya Wiki, Real walibwagwa nje ya Copa del Rey walipotoka 2-2 na Celta Vigo baada ya kufungwa Mechi ya Kwanza 2-1.
Hata
hivyo, kwenye La Liga, Real, chini ya Kocha Zinedine Zidane, wapo
Pointi 1 mbele ya Sevilla na 2 mbele ya Barcelona huku wao wakiwa
wamecheza Mechi 1 pungufu.
Kuporomoka
kwa fomu ya Real kumeandamwa na kuwa na Majeruhi 7 kwenye Kikosi chao
cha Kwanza ambao ni Raphael Varane, Gareth Bale, James Rodriguez, Luka
Modric, Marcelo, Dani Carvajal na Pepe ingawa Varane huenda akacheza
Mechi na Sociedad.
Nao
Real Sociedad watatinga kwenye Mechi hii na Real huko Santiago Bernabeu
wakitoka kwenye kichapo cha 5-2 toka kwa Barcelona kwenye Mechi ya Copa
del Rey.
Jumapili
Barcelona watacheza Mechi yao mapema Ugenini na Real Betis na ushindi
kwao utawafanya waongoze La Liga kwa muda kwa vile Real na Sevilla
watacheza Mechi zao baadae.
0 Maoni:
Post a Comment