LA LIGA: RONALDO AIPAISHA REAL POINT 4 MBELE YA BARCA. SEVILLA….NA 1 MKONONI!

Tokeo la picha la goli la ronaldo la jana image
VINARA wa La Liga Real Madrid wamepaa kileleni wakiwa Pointi 4 mbele na Mechi 1 mkononi baada ya Jana kuitwanga Real Sociedad 3-0 wakati Wapinzani wao Barca wakidroo na Sevilla kufungwa.

Real sasa wamecheza Mechi 19 na wana Pointi 46 wakati Barca na Sevilla, zilizocheza Mechi 20 kila moja, zina Pointi 42 kila moja.

Bao za Real hapo Jana Uwanjani kwao Santiago Bernabeu zilipigwa na Mateo Kovacic akipokea msaada wa Cristiano Ronaldo katika Dakika ya 38 na kisha Dakika ya 51 Kovacic kumtengenezea Ronaldo aliepiga la Pili, likiwa Bao lake la 13 katika Mechi 13 zilizopita, na la 3 kuingizwa Dakika ya 82 kupitia Alvaro Morata alieunganisha Krosi ya Lucas Vazquez.

Real Sociedad walicheza Mtu 10 kuanzia Dakika ya 74 baada ya Inigo Martinez kuzoa Kadi za Njano 2 na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.

**La Liga Ratiba**
Jumatatu Januari 30
2245 Las Palmas v Valencia
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment