LEWANDOWSKI, CAVANI, KANE NA HIGUAN WAMPA CHANGAMOTO MARCUS RASHFORD.

Unaweza kusema safari ndiyo imeanza na kutakuwa na mwamko wa kujichangamsha kwa mshambuliaji kinda wa Man United, Marcus Rashford.

Jana alikuwa katika kundi la wachezaji waliokwenda kupiga picha kutengeneza matangazo ya Nike.


Rashford na wakongwe wengine Robert Lewandowski, Marcus Rashford, Harry Kane, Gonzalo Higuain na Edinson Cavani jumla wamefunga mabao 81 msimu huu, lakini yeye akiwa na mabao sita tu.

Kwake ni kama deni, lakini kupata nafasi ya kuwa na watu hao wa kazi, ni changamoto kwamba safari yake ni ndefu na anatakiwa kupambana hasa.

Bado hana nafasi ya uhakika katika kikosi cha Man United chini ya Kocha Jose Mourinho, hivyo anatakiwa kupambana kwelikweli.


MABAO YAO WOTE:
Robert Lewandowski - 20
Marcus Rashford - 6
Harry Kane - 15
Gonzalo Higuain - 16
Edinson Cavani - 24 
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment