Klabu ya West Ham imeamua kumwaga mboga baada ya kukataa ofa ya pauni million 22 kutoka kwa klabu ya Marseille ya Ufaransa.
Marseille imetoa ofa hiyo ili kumpata kiungo Mfaransa Dimitri Payet.
Hata hivyo West Ham imeweka msisitizo kwamba Payet hatakwenda popote Januari hii, maana yake haina mpango wa kumuuza.
Hii
imetokea baada ya siku chache zilizopita Payet kugoma kufanya mazoezi
akishinikiza kuuzwa hali iliyosababisha mashabiki kumzomea kila
wanapomuona au kuziona picha zake.
Pamoja
na West Ham kuweka msisitizo huo, Rais wa Marseille, Jacques-Henri
Eyraud ametua jijini London kuangalia kama anaweza kulimaliza suala hilo
kwa kuzungumza na bosi wa West Ham, David Sullivan.
David Sullivan. |
0 Maoni:
Post a Comment