Hii ni kwa mara ya kwanza Man U kuongoza tokea mwaka 2004 |
Timu ya Manchester
United imepata kipato kikubwa kuliko timu yoyote katika msimu uliopita
kulingana na taarifa zilizochapishwa na kampuni kubwa ya ukaguzi duniani
(Deloitte).
Manchester United imewashinda Real Madrid waliofanya
vizuri katika michezo kwa miaka 11baaada ya kukusanya kipato kikubwa
takribani Euro 689 katika msimu wa 2015-2016.
Clubu za ligi ya Premier imeshuhudia kukua kwa kipato kwa Euro Millioni mia moja.
Mauzo makubwa ya jezi ni moja ya chanzo cha mapato kwa United |
Ukijumlisha vipato vya timu ishirini bora kwa msimu
wa 2015-2016 vimeongezeka kwa asilimia 12% na kufikia euro billioni 7.4
hii haijawahi kutokea.
Hii ni mara ya kwanza kwa Man U kushikilia nafasi hiyo tokea msimu wa 2003-04.
Barcelona inasalia nafasi ya pili |
Real Madrid wameshuka mpaka nafasi ya tatu wakiwaacha wapinzani wao wakubwa Barcelona katika nafasi ya pili.
![]() |
Madrid imeshuka mpaka nafasi ya tatu |
Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wapo nafasi ya
nne huku matajiri wa jiji la Manchester Man City wakiwa nafasi ya tano
kwa kutengeneza Euro milioni524 kwa msimu uliopita.
Hii ni mara ya kwanza kwa city kuingia katika nafasi hiyo.
Msimamo kwa Mapato Orodha ya Deloitte 2015-16 KUMI BORA | ||
---|---|---|
Klabu (Nafasi msimu uliopita) | Mapato kwa €m (£m kwenye mabanos) 2015-16 | Mapato 2014-15 |
1 (3) Manchester United | 689 (515.3) | 519.5 (395.2) |
2 (2) Barcelona | 620.2 (463.8) | 560.8 (426.6) |
3 (1) Real Madrid | 620.1 (463.8) | 577 (439) |
4 (5) Bayern Munich | 592 (442.7) | 474 (360.6) |
5 (6) Manchester City | 524.9 (392.6) | 463.5 (352.6) |
6 (4) Paris St-Germain | 520.9 (389.6) | 480.8 (365.8) |
7 (7) Arsenal | 468.5 (350.4) | 435.5 (331.3) |
8 (8) Chelsea | 447.4 (334.6) | 420 (319.5) |
9 (9) Liverpool | 403.8 (302) | 391.8 (298.1) |
10 (10) Juventus | 341.1 (255.1) | 323.9 (246.4) |
0 Maoni:
Post a Comment