Manchester United, ikiongozwa na Meneja Jose
Mourinho, wamepiga hatua kubwa kuelekea kutwaa Taji kubwa la pili Msimu
huu baada ya Jana huko kwao Old Trafford kuichapa Hull City 2-0 katika
Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali ya EFL CUP, ambalo ndio Kombe la Ligi
huko England.
Mwanzoni mwa Msimu, Man United walitwaa Ngao ya Jamii.
Bao za Man United, waliochezesha karibu Kikosi chao chote, zilifungwa na Juan Mata na Marouane Fellaini alieanzia Benchi.
Bao
la Mata lilifungwa Dakika ya 56 alipounganisha Kichwa cha Henrikh
Mkhitaryan na la pili Dakika ya 87 kupitia Fellaini alieunganisha Krosi
ya Matteo Darmian.
Hull City na Man United zitarudiana huko KCOM Stadium hapo Januari 28.
Leo Jumatano Januari 11 itachezwa Nusu Fainali ya Pili huko Saint Mary kwa Southampton kucheza na Liverpool.
Nusu
Fainali hizi huchezwa kwa Mikondo Miwili ya Nyumbani na Ugenini na
hivyo Marudiano ya Mechi hizi yatakuwa hapo Januari 25 na 26 huko
Anfield na KCOM Stadium.
EFL CUP
Nusu Fainali.
Ratiba/Matokeo:
Jumanne Januari 10
Manchester United 2 Hull City 0
Jumatano Januari 11
**Saa za Bongo
2245 Southampton V Liverpool
0 Maoni:
Post a Comment