SIMBA YAENDELEA KUFUTA UTEJA KWA WAPINZANI WAO YANGA.

Tokeo la picha la SIMBA VS YANGA MAPINDUZI CUP IMAGE
Nusu Fainali ya Pili ya Kombe la Mapinduzi ambayo ni Mashindano ya kuenzi Miaka 53 ya Mapinduzi Tukufu ya Visiwa vya Zanzibar na Pemba, iliyokuwa Bigi Mechi, Dabi ya Kariakoo iliyohamia Amaan Stadium Zanzibar. Ilichezwa Jana Usiku na Simba na Yanga kutoka 0-0 katika Dakika 90 lakini Simba kuibuka kidedea kwa Mikwaju ya Penati 4-2 na kutinga Fainali watakayocheza na Azam FC.
 
Katika Nusu Fainali nyingine iliyochezwa mapema Jana Taifa Jang’ombe ya Zanzibar ilifungwa 1-0 na Azam FC kwa Bao la Dakika ya 33 la Frank Domayo.

Kwenye Mechi ya Watani wa Jadi, Timu zote zilishambuliana kwa zamu ingawa Yanga walionekana kutawala zaidi bila matunda yeyote na Gemu kuamuliwa kwa Mikwaju ya Penati Tano Tano.
 

Katika Penati hizo, Simba walifunga kupitia Kepteni wao Jonas Mkude, Kipa Daniel Agyei, Muzamil Yasin na Bokungu wakati ile iliyopigwa na Mwanjali kuokolewa na Kipa wa Yanga Munishi.

Penati za Yanga zilifungwa na Simon Msuva na Thabani Kamusoko na zile za Kipa Munishi na Mwinyi Haji ziliokolewa na Kipa wa Simba Daniel Agyei.

Fainali ya Mapinduzi Cup itachezwa Ijumaa Januari 13.

VIKOSI VILIVYOANZA:

YANGA: Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Haji, Andrew Vincent ‘Dante’, Kelvin Yondan, Saidi Juma ‘Makapu’, Simoni Msuva, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe, Haruna Niyonzima, Deusi Kaseke 

SIMBA: Daniel Agyei, Janvier Bokungu, Mohamed Hussein 'Tshabalala', Abdi Banda, Method Mwanjali, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, James Kotei, Juma Luizio, Muzamil Yassin, Mohamed Ibrahim
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment