Mchezaji
wa Manchester City Bacary Sagna amefunguliwa Mashitaka na FA, Chama cha
Soka England, kuhusu Posti yake Mtandaoni Instagram alipohoji umakini
wa Refa Lee Mason na wakati huo huo Rufaa ya Nahodha wa Chelsea John
Terry atatumikia Kifungo baada ya Rufaa yake kupinga Kadi Nyekundu
kutupiliwa mbali.
Sagna aliandika kwenye Instagram: “10 dhidi ya 12…lakini tulipigana na tulishinda kama Timu!”
Posti
hiyo ilitoka mara baada ya City kuifunga Burnley 2-1 Wiki iliyopita
huko Etihad Stadium kwenye Mechi EPL, Ligi Kuu England, ambayo City
walibaki Mtu 10 kuanzia Dakika ya 32 kufuatia Kiungo wao Fernandinho
kutolewa kwa Kadi Nyekundu na Refa Lee Mason kufuatia Rafu mbaya.
Sheria za FA zinakataza Posti kwenye Mitandao ya Kijamiii zinazohoji uadilifu wa Marefa.
Sagna, ambae ameomba radhi kuhusu Posti hiyo, amepewa hadi Saa 3 Usiku, Saa za Bongo, Ijumaa Januari 13 kujibu Shitaka lake.
WAKATI HUO HUO, Rufaa ya Nahodha wa Chelsea John Terry kupinga Kadi Nyekundu aliyopewa Jumapili walipocheza na Peterborough kwenye FA CUP imegonga mwamba na sasa atatumikia Kifungo cha Mechi 1.
Adhabu hii itamfanya Terry aikose Mechi ya EPL dhidi ya Mabingwa Watetezi Leicester City hapo Jumamosi.
FA
pia imethibitisha Beki wa Middlesbrough, Klabu ya EPL maarufu kama
Boro, Daniel Ayala atatumikia Kifungo cha Mechi 3 baada ya Rufaa kupinga
Kadi Nyekundu aliyopewa kwenye Mechi ya FA CUP na Sheffield Wednesday
Wikiendi iliyopita kutupwa.
0 Maoni:
Post a Comment