RAIS WA FIFA Gianni Infantino |
FAINALI za Kombe la Dunia zitapanuliwa na kushirikisha Nchi 48 kutoka 32 za hivi sasa.
Mabadiliko hayo yamepitishwa jana huko Zurich, Uswisi kwa Kura
nyingi na yataanza kwenye Fainali za Mwaka 2026 ambazo bado hazijapata
Mwenyeji.
Fainali zijazo zitachezwa huko Russia Mwaka 2018 na zinazofuata ni huko Qatar Mwaka 2022 na zote zitakuwa na Timu 32 tu.
Kwenye Mfumo wa Timu 48 kwenye Fainali, Mechi za Awali zitakuwa za
Makundi 16 ya Timu 3 kila moja ambayo yatatoa Timu 32 kwenda Raundi ya
Mtoano.
************************************************************
FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA - Timu 48:
- Makundi: Mechi 2
- Raundi ya Mtoano ya Timu 32
- Raundi ya Mtoano ya Timu 16
- Robo Fainali
- Nusu Fainali
- Fainali
************************************************************
Kwa Mfumo huo mpya Jumla ya Mechi kwenye Fainali zitakuwa 80 kutoka
64 za sasa lakini Bingwa wa Dunia atacheza Mechi 7 tu kama ilivyo sasa
ambazo zote zitakamilika ndani ya Siku 32.
Hii ni mara ya kwanza kwa FIFA kuongeza idadi ya Timu kwenye
Fainali za Kombe la Dunia tangu zilipopanuliwa Mwaka 1998 na kuwa za
Timu 32 kutoka 24.
Kwa mujibu wa tafiti za FIFA upanuzi huu utafanya Mapato yaongezeke
na kuwa Pauni Bilioni 5.29 na kuleta Faida kuwa Pauni Milioni 521.
0 Maoni:
Post a Comment