Mechi ya watani Simba Vs Yanga inapigwa leo na hilo ndiyo gumzo la kila sehemu hasa unapozungumzia mchezo wa soka.
Simba inaivaa Yanga katika mechi nusu fainali ya ya Kombe la Mapinduzi kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.
Mara nyingi mashabiki wa soka wanakuwa ni watu wanaoamua wanachokiamini hata kabla mpira haujachezwa.
Wengi
sana wamekuwa wakiamini Yanga itapoteza mchezo huo, kinachowafanya
waamini Yanga itapoteza ni kwa kuwa tu ilifungwa mabao 4-0 dhidi ya Azam
FC katika mechi iliyopita.
Hilo ni kosa kubwa sana kwa kuwa Yanga imepoteza lakini ndiyo timu iliyokuwa inafanya vizuri zaidi ya timu nyingine.
Kabla
ya kufungwa na Azam FC, Yanga iliitwanga Jamhuri kwa mabao 6-0, halafu
wakaifunga Zimamoto 2-0 kabla ya kukutana na gharika ya Azam FC.
Utaangalia
kawa kabla, safu ya ulinzi ya Yanga katika mechi mbili haikuwa
imeruhusu bao, ikafanya makosa na ikaruhusu mabao manne katika mechi
moja.
Katika
mechi mbili, Yanga walikuwa wamefunga mabao nane na kuwa wenye mabao
mengi zaidi ya timu nyingine, katika mechi hiyo moja dhidi ya Azam
wakashindwa kufunga.
Yanga
ina wachezaji wazoefu na wanaoujua mpira hasa ukizungumzia kwa kiwango
cha soka hapa nchini. Maana yake wana nafasi kubwa ya kujirekebisha
wakiyatumia makosa dhidi ya Azam FC.
Kama wana uwezo wa kujirekebisha, maana yake kuna nafasi kubwa sana ya kufanya vizuri.
Simba
wana kikosi kizuri ambacho wamekuwa makini sana. Licha ya ushindi wa
bao chache lakini wanaonekana ni wenye malengo na wamejipanga wanataka
nini.
Kikubwa cha kuamini kuwa mchezo wa leo ni mgumu hasa kwa kila timu na kila mmoja lazima awe makini sana.
Simba
wanataka kuendeleza ushindi wa mechi zote kama walivyoanza, Yanga
wanataka kujirekebisha na huenda ndiyo wakawa hatari zaidi kwa kuwa
hawatakubali kufungwa mara mbili.
0 Maoni:
Post a Comment