Mshambuliaji Ibrahim Ajibu ni kati ya walio tayari kwa ajili ya mechi yao watani wao Yanga, leo.
Simba inaivaa Yanga katika mechi nusu fainali ya ya Kombe la Mapinduzi kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.
Ajibu
ambaye amerejea nchini wiki iliyopita baada ya kufanya majaribio Haras
El Hodood, ameanza mazoezi na wenzake na yuko tayari kwa ajili ya mechi
ya leo.
“Ajibu naye yuko fiti, hapa ni chaguo la mwalimu Omog kama atamhitaji,” kilieleza chanzo.
Hata
hivyo, kinachoonekana ni chaguo kubwa alilonalo Kocha Joseph Omog kwa
kuwa pamoja na Ajibu, wako akina Mohamed Ibrahim, Pastory Athanas, Juma
Luizio, Shiza Kichuya na wegine wengi.
0 Maoni:
Post a Comment