Mshambuliaji wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic ameshinda kesi
ya kukashifiwa kwa tuhuma za kutumia dawa za kuongeza nguvu.
Mahakama ya Sweden imemuamuru kocha wa mbio, Ulf Karlsson kulipa
faini ya pauni 2500 kwa kutoa kauli za kumtuhumu nyota huyo wa Sweden
kutumia dawa za kuongeza nguvu wakati akiwa Juventus.
Karlsson aliyekuwa kocha wa timu za mbio za Sweden kati ya mwaka 2001
na 2004 alidai mwaka jana kuwa Ibrahimovic atakuwa alikuwa akitumia
dawa za kuongeza nguvu kukuza misuli yake.
” Misuli ya Zlatan iliongezeka kwa kilo 10 ndani ya miezi 6 akiwa
Juventus. Hio haiwezekani katika kipindi hicho kidogo.” Alidai Karlsson
mbele ya jopo kabla ya kuongezea kuwa, ” Nafikiri alikuwa anatumia
madawa. Nashawishika kuamini hivyo. ”
Mahakama imejiridhisha kuwa kauli hio japokuwa haitaji moja kwa moja
kuwa Ibrahimovic anatumia dawa za kuongeza nguvu bado inaashiria kashfa
kwa nyota huyo hivyo kumtoza faini Karlsson.
0 Maoni:
Post a Comment