LEO
zipo Mechi Mbili za Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi ambayo ni
Mashindano ya kuenzi Miaka 53 ya Mapinduzi Tukufu ya Visiwa vya Zanzibar
na Pemba, lakini macho, masikio na kila hisia ni Bigi Mechi wakati Dabi
ya Kariakoo ikihamia Amaan Stadium Zanzibar kwa Yanga kupambana na
Watani zao Simba.
Nusu
Fainali nyingine hii Leo ni kati ya Watoto wa Nyumbani Taifa Jang’ombe,
waliowatoa waliokuwa Mabingwa Watetezi URA ya Uganda, na Azam FC.
Wakati
Kambi ya Simba ni shwari baada ya kushinda Mechi 3 na Sare 1 kwenye
Kundi A, Yanga kuna walakini baada kushinda Mechi zao 2 za kwanza za
Kundi B kwa kishindo na kufuzu lakini wakatandikwa 4-0 na Azam FC katika
Mechi yao ya mwisho ya kukamilisha Ratiba Kundini.
Msukukosuko
huo umemfanya Kocha Mkuu wa Yanga kutoka Zambia, George Lwandamina,
kukiri hali ni ngumu kwao na hasa kutokana na Majeruhi ambao wataikosa
Mechi na Simba ambao ni Straika Amissi Tambwe kutoka Burundi, Wazambia
wao Wawili, Justin Zulu na Obrey Chirwa, na Mzimbabwe Donald Ngoma.
Hata
hivyo, Kocha huyo amesisitiza wataingia na kupigana kiume kwa Kikosi
kilichobaki huku Historia ya Dabi hii ikidhihirisha Miaka nenda rudi
Ubora wa Timu si kigezo kwani yeyote anaweza kushinda mtanange kati yao
ikiwa Karata zitachangwa vizuri ndani ya Dakika 90 za Mechi.
Yanga na Simba zimekutana Amaan Stadium, Zanzibar mara 4. Pata kumbukumbu:
- Mechi ya Kwanza 1975
Mwaka
1975, Yanga iliichapa Simba 2-0 kwenye Fainali ya Klabu Bingwa Afrika
Mashariki na Kati kwa Bao za Gibson Sembuli na Sunday Manara.
- Mechi ya Pili 1992
Simba
ilishinda Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati kwa Mikwaju
ya Penati 6-5, baada ya Sare ya 1-1 katika Dakika 120 ambayo Simba
ilitangulia kufunga kwa Bao la Hussein Masha na Yanga kurudisha kupitia
Saidi Mwamba ‘Kizota’,
- Mechi ya Tatu 1992
Bao pekee la Daniel Kimti liliipa Simba ushindi wa 1-0 katika Nusu Fainali ya Kombe la Muungano.
- Mechi ya Nne 2011
Simba ilishinda 2-0 kwenye Fainali ya Kombe la Mapinduzi kwa Bao za Shija Mkina na Mussa Hassan ‘Mgosi;.
MSIMAMO:
KUNDI A
NA | TIMU | P | W | D | L | F | A | GD | PTS |
1 | SIMBA | 4 | 3 | 1 | 0 | 5 | 1 | 4 | 10 |
2 | TAIFA JANG’OMBE | 4 | 3 | 0 | 1 | 6 | 3 | 3 | 9 |
3 | JANG’OMBE BOYS | 4 | 2 | 0 | 2 | 5 | 5 | 0 | 6 |
4 | URA | 4 | 1 | 1 | 2 | 3 | 3 | 0 | 4 |
5 | KVZ | 4 | 0 | 0 | 4 | 2 | 9 | -7 | 0 |
KUNDI B
NA | TIMU | P | W | D | L | F | A | GD | PTS |
1 | AZAM | 3 | 2 | 1 | 0 | 5 | 0 | 5 | 7 |
2 | YANGA | 3 | 2 | 0 | 1 | 8 | 4 | 4 | 6 |
3 | ZIMAMOTO | 3 | 1 | 0 | 2 | 2 | 3 | -1 | 3 |
4 | JAMHURI | 3 | 0 | 1 | 2 | 0 | 8 | -8 | 1 |
Nusu Fainali
Azam FC v Taifa Jang’ombe (Saa 10: 00 jioni)
Simba v Yanga (Saa 2:15 Usiku)
Ijumaa, Januari 13, 2017
FAINALI
Saa 2: 15 Usiku
Azam FC/Taifa Jang’ombe v Simba/Yanga
0 Maoni:
Post a Comment