DROO
YA RAUNDI YA 4 ya EMIRATES FA CUP imefanyika Usiku wa kuamkia leo huko BT Tower
Mjini London ikiendeshwa na Wachezaji wa zamani wa Kimataifa wa England
Michael Owen na Martin Keown na Mabingwa Watetezi Manchester United
kupangwa kucheza kwao Old Trafford na Wigan Athletics.
Man
City na Arsenal zote zimepangwa kucheza Ugenini kwa Arsenal kuivaa
Southampton au Norwich na Man City kucheza na Mshindi kati ya Crystal
Palace na Bolton.
Liverpool, kama wataifunga Plymouth katika Mechi yao ya Marudiano baada ya Sare, watakuwa kwao Anfield kucheza na Wolves.
Vinara wa Ligi Kuu England, Chelsea, wao wako kwao Stamford Bridge kuivaa Brentford.
Mabingwa
Watetezi wa Ligi Kuu England, Leicester City, watacheza Ugenini na
Derby County wakati Tottenham wakicheza Nyumbani White Hart Lane na
Wycombe.
JE UNALIJUA HILI KUHUSU LA EMIRATES FA CUP?
- FA CUP 2016/17, ambalo pia hujulikana kama FA Challenge Cup, ni mara ya 136 kushindaniwa kila Mwaka tangu lilipoanzishwe na linatambuliwa kama ndio Mashindano ya kale kupita yote Duniani.
- Kombe hili linadhaminiwa na Kampuni ya Ndege8k ya Emirates na kwa sababu za kiudhamini linaitwa Emirates FA Cup.
- Timu 736 zilikubaliwa kushiriki Mashindano haya Msimu huu na yalianza kwa Raundi ya Awali na yatafikia Tamati kwa Fainali itakayochezwa Uwanjani Wembley Jijini London hapo Mei 27, 2017.
- Mshindi wa FA CUP ataingizwa Hatua ya Makundi ya UEFA EUROPA LIGI Msimu wa 2017/18.
0 Maoni:
Post a Comment