HAKUNA UBISHI KUWA CHRISTIANO RONALDO NI BORA DUNIANI KWA SASA

 FIFA-BEST-RONALDO

HAFLA ya FIFA ya kutunuku Tuzo za FIFA za Ubora Duniani kwa Mwaka 2016 zimefanyika Usiku wa kuamkia leo huko Zurich, Uswisi na Cristiano Ronaldo kuibuka ndio Mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani.
 
Akitwaa Tuzo hii, Ronaldo, anaechezea Real Madrid na Nchi yake Portugal, aliwashinda kwa Kura Lionel Messi na Antoine Griezmann.

Ronaldo pia alitwaa, mapema Mwezi Desemba, Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani kwa 2016, Ballon d’Or, inayotolewa na Jarida la France, France Football, Tuzo ambayo kabla ya hapo, kwa Miaka 6, iliunganishwa na FIFA na kuitwa FIFA Ballon d’Or, lakini kuanzia safari hii wametengana.

Kwa upande wa Kinamama, Mchezaji Bora ni Carli Lloyd wa USA.

Kocha Bora Duniani kwa Wanaume ni Claudio Ranieri baada ya kuiwezesha Leicester City, bila kutegemewa, kutwaa Ubingwa wa England kwa mara ya kwanza katika Historia yao.

Nae Mohd Faiz Subri wa Penang, Malaysia ndie alitwaa Tuzo ya Puskas ya Goli Bora la Mwaka.

Kwenye Tuzo ya Mashabiki, Mashabiki wa Timu za Liverpool na Borussia Dortmund, kwa pamoja, wameshinda Tuzo hii kwa tukio la kuimba wote ‘Wimbo wa Taifa wa Liverpool’ -'You'll Never Walk Alone'- Uwanjani Anfield kabla ya Mechi yao ya Robo Fainali ya UEFA EUROPA LIGI Msimu uliopita.

FIFA-BEST-RANIERI

FIFA TUZO ZA UBORA – WAGOMBEA NA MSHINDI:
MCHEZAJI BORA WANAUME:
  • Wagombea: Cristiano Ronaldo, Antoine Griezmann, Lionel Messi
  • Mshindi: Cristiano Ronaldo

MCHEZAJI BORA WANAWAKE:
  • Wagombea: Melanie Behringer, Carli Lloyd, Marta
    Tokeo la picha la Carli Lloyd wa USA image
  • Mshindi: Carli Lloyd wa USA.

KOCHA BORA WANAUME:
  • Wagombea: Claudio Ranieri, Fernando Santos, Zinedine Zidane
  • Mshindi: Claudio Ranieri wa Mabingwa wa England Leicester City
KOCHA BORA WANAWAKE:
  • Wagombea: Jill Ellis, Silvia Neid, Pia Sundhage
  • Mshindi: Silvia Neid [Germany]
GOLI BORA [Tuzo ya Puskas]:
  • Wagombea: Marlone, Daniuska Rodriguez, Mohd Faiz Subri
  • Mshindi: Mohd Faiz Subri wa Penang, Malaysia.
**Tuzo hii inatokana na Kura za Mashabiki Duniani kote.

TUZO TOKA KWA MASHABIKI:
  • Wagombea: Mashabiki wa Den Haag, Borussia Dortmund & Liverpool na Iceland.
  • Mshindi: Mashabiki wa Borussia Dortmund & Liverpool
TUZO YA UCHEZAJI WA HAKI
  • Mshindi: Atletico Nacional ya Colombia
  •  
FIFA FIFPro World11 2016
  • Kikosi Bora cha Mwaka 2016:
-Kipa: Neur
-Mabeki: Alves, Pique, Ramos, Marcelo
-Viungo: Modric, Kroos, Iniesta
-Mafowadi: Suarez, Ronaldo, Messi
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment