MANCHESTER UNITED INAWAKARIBISHA HULL CITY KWENYE EFL LEO

Tokeo la picha la efl cup image

NUSU FAINALI za Kombe la Ligi huko England ambalo sasa huitwa EFL CUP (English Football League Cup) zitaanza leo Jumanne Januari 10 huko Old Trafford kwa Manchester United kucheza na Hull City.

Siku ya Pili, Jumatano Januari 11, itachezwa Nusu Fainali ya Pili huko Saint Mary kwa Southampton kucheza na Liverpool.
Nusu Fainali hizi huchezwa kwa Mikondo Miwili ya Nyumbani na Ugenini na hivyo Marudiano ya Mechi hizi yatakuwa hapo Januari 25 na 26 huko Anfield na KCOM Stadium.
Kwenye Mechi ya Old Trafford, Meneja wa Man United Jose Mourinho amedokeza atabadili Kikosi chake toka kile kilichoichapa Reading 4-0 Jumamosi katika Raundi ya 3 ya FA CUP.
Akiongea baada ya Mechi hiyo, Mourinho alieleza: "Jumamosi tumecheza na Wachezaji freshi. Ila sitaki ieleweke tuna Timu ya Kwanza au ya Pili! Wachezaji ambao hawakucheza Mechi hii watacheza na Hull..hivyo ni rahisi kujua Zlatan, Pogba, Herrera, Valencia watarudi Mechi na Hull."

 Tokeo la picha la man u vs hull city efl cup
******************************************************
JE WAJUA KWAMBA?
  • Msimu huu hili Kombe la Ligi halina Mdhamini na limebatizwa English Football League Cup, EFL CUP.
  • Huko nyuma Kombe la Ligi, kwa sababu za kiudhamini, liliwahi kubatizwa Coca-Cola Cup, Worthington Cup, Carling Cup na Capital One Cup.
*******************************************************
Hull City, chini ya Meneja Mpya Marco Silva kutoka Ureno alietwaa mikoba ya Mike Phelan alietimuliwa Wiki iliyopita, itatinga Old Trafford ikiwa na Difensi ya kuungaunga kutokana na Majeruhi kadhaa.
Sentahafu wao Michael Dawson aliumia na kutolewa Kipindi cha Pili Juzi kwenye FA CUP walipoifunga Swansea City na nafasi hiyo kushikwa na Kiungo Tom Huddlestone alishirikiana na Kiungo mwingine Jake Livermore.
Beki mwingine Majeruhi wa Hull ni Curtis Davis na hivyo kuwaacha Hull kutumia Viungo Watatu kwenye Nafasi 4 za Difensi yao.
Nafasi ya Fulbeki wa Kulia imelazimika kuzibwa na David Meyler baada ya kumpoteza Ahmed Elmohamady ambae ameenda Egypt kujiunga na Timu ya Taifa kwa ajili ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2017, yanayoanza huko Gabon Januari 14.
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment