Kipa
aliyekuwa akikipiga kwenye kikosi cha Simba, Vincent Angban, ameibuka
na kusema amesamehe kila kitu kilichotokea kwenye klabu hiyo ikiwemo
madai yake baada ya kuvunjiwa mkataba.
Angban,
kwenye usajili wa dirisha dogo msimu huu alisitishiwa mkataba wake
uliobaki wa miezi sita ambapo aliahidiwa kulipwa mshahara wake wa mwezi
mmoja baada ya makubaliano ya kuvunjwa mkataba huo.
Taarifa
kutoka ndani ya Simba, zinasema Angban alitakiwa kulipwa dola 1,000
ambazo ni zaidi ya Sh milioni 2 alizokuwa akichukua kila mwezi.
Kwa
mujibu wake, mpaka anaondoka nchini mwishoni mwa mwaka jana, alikuwa
hajalipwa kitu, hivyo ameamua kutofuatilia wala kuzungumzia madai hayo
tena.
Akizungumza
kutoka kwao nchini Ivory Coast, Angban alisema: “Sipendi kuzungumzia
ishu ya madai yangu na Simba baada ya mkataba kuvunjwa kwa sababu
nimeamua kusamehe kila kitu, kwa sasa nimeamua kutafuta maisha sehemu
nyingine na siku si nyingi nitarudi uwanjani.
“Nipo nyumbani Ivory Coast nikijifua mwenyewe, kila siku nimekuwa nikifanya mazoezi ya gym ili kujiweka sawa huku nikisikilizia timu ya kujiunga nayo kwani kwa sasa usajili bado haujafunguliwa na kuna timu zinanihitaji, dili likikamilika nitakwambia nimejiunga na timu gani."
0 Maoni:
Post a Comment