TP Mazembe imefanikiwa kumrudisha kundini
nyota wake wa zamani, Tresor Mputu baada ya kushinda kesi dhidi ya klabu
ya Kabuscorp ya Angola.
Mputu alishindwa kucheza kwa muda mrefu baada ya kuondoka Kabuscorp ambayo ilidai amevunja mkataba.
Baada ya juhudi kubwa za rais wa TP Mazembe, Moise Katumbi ambaye
alituma wawakilishi wake FIFA, Mputu ameishinda kesi hio na Kabuscorp
wameamuliwa kuwalipa TP Mazembe dola milioni 1.5 iliyokuwa ada ya
uhamisho wake.
FIFA imeliarifu shirikisho la mpira la JK Kongo, FECOFA kumuidhinisha Mputu kuichezea TP Mazembe kwa mara nyingine.
Mputu anakumbukwa na wengi kwa kuiongoza TP Mazembe kuwa klabu ya
kwanza Afrika kufika fainali za Klabu Bingwa Duniani mwaka 2010
walipofungwa na Inter Milan.
Kwa upande mwingine, TP Mazembe imewaongezea mikataba nyota wake, Jonathan Bolingi na Rainford Kalaba.