WAJUE VIUNGO WATANO HATARI KWA KUZIFUMANIA NYAVU VPL

 Tokeo la picha la Ally Nassor ‘Ufudu’-Kagera Sugar IMAGE
Msimu huu wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara 2016/17, kumekuwa na vita kali ya mastraika, mawinga na viungo wa kati katika kushindana kufunga magoli.

Straika, Amissi Tambwe wa Yanga, mshindi wa kiatu cha dhahabu msimu uliopita, tayari amefikisha mabao tisa.
Straika mwenzake, John Bocco anayeichezea Azam, mshindi wa kiatu cha dhahabu msimu wa Ligi Kuu 2011/12 anafuatiwa akiwa na magoli manane.

Rashid Mandawa wa Mtibwa Sugar na Donald Ngoma wa Yanga, ni mastraika ambao wana magoli saba kila mmoja.
Hawa wana ushindani mkali kutoka kwa mawinga, Shiza Kichuya wa Simba na Simon Msuva wa Yanga. Mawinga hawa wa kulia, wote wanakabana koo na Tambwe akiwa wamefunga magoli tisa kila mmoja.

Kama vile haitoshi, kuna viungo wa kati ambao msimu huu nao wanaonekana wamekuja juu mno kwenye kupachika mabao na kufanya vita wa kugombea ufungaji bora kuwa ya ushindani mkali na ya kusisimua.

Kwa muda mrefu kwenye Ligi Kuu ya Tanzania, wanaochukua ufungaji bora ni mastraika, na kama si wao basi ni mawinga, kama ilivyokuwa kwa Mrisho Ngasa, msimu wa 2010/11, Kipre Tchetche 2012/13 na Simon Msuva, 2014/15.

Kama viungo wa kati waliocharuka msimu huu kutupia wakiendelea hivi, huenda kwa mara ya kwanza, idara hiyo ikatoa mfungaji bora.
************************************************************
1. Mzamiru Yassin-Simba
Tokeo la picha la MUZAMIRU YASSIN IMAGE
Yassin Muzamiru







Ni kiungo wa kati wa Simba, aliyesajiliwa msimu huu akitokea Mtibwa Sugar. Anawaongoza viungo wa kati kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara kufunga magoli mengi zaidi. Na huyu ndiye anayeonekana kuwaweka roho juu zaidi wanaoongoza kwenye orodha ya wafungaji mpaka sasa.
Ameshafunga magoli sita mpaka sasa, akiwa amezidiwa magoli matatu tu na wanaoongoza. Kasi yake kwenye ufungaji ni ya kutisha na amekuwa msaada kwa timu yake ya Simba, kwani hata kwenye Kombe la Mapinduzi, tayari ameshafunga magoli mawili mpaka sasa.
************************************************************
2. Rafael Daudi-Mbeya City

Rafael-AlphaF (1)

Ni kiungo wa kati ambaye amekuwa kwenye kiwango bora kabisa kwa msimu wa tatu sasa. Mbali na kuiunganisha vema timu yake na kuwalisha mastraika, amekuwa na uwezo mkubwa wa kupachika mabao na kuibeba mara kwa mara timu yake ya Mbeya City kwenye mechi ngumu.
Ameshapachika mabao matano mpaka sasa kwenye Ligi Kuu na kwa mwendo anaoendelea nao, ni tishio kwa wafungaji wengine.
************************************************************
3. Ally Nassor ‘Ufudu’-Kagera Sugar
Ni mmoja kati ya viungo wenye uwezo wa hali ya juu kwa sasa. Msimu huu anaichezea Kagera Sugar.
Ameshafunga magoli matatu mpaka sasa. Amekuwa ni kiungo mwenye uwezo mkubwa wa kufunga magoli kwenye mechi za Ligi Kuu.
 ***********************************************************
4. Shaaban Kisiga-Ruvu Shooting
Huenda akawa kiungo mkongwe zaidi kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu. Ameshawahi kuichezea Simba kwenye vipindi viwili tofauti.
Mpaka sasa ameshaifungia timu yake ya Ruvu Shooting mabao matatu. Ni mmoja wa viungo wenye uwezo mkubwa wa kufunga magoli, na hasa ya mipira iliyokufa.
************************************************************
5. Jamal Sudi-Toto Africans
Huyu ni kiungo wa kukaba. Anaichezea Toto Africans. Lakini ameondokea kuwa mfungaji mzuri sana msimu huu.
Ameshaifungia timu yake mabao matatu mpaka sasa na kuwa kwenye orodha ya viungo wa kati wenye uwezo wa kupachika mabao kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.
************************************************************
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment