BARCELONA YANUSURIKA KUCHAPWA.

 www.kiungomshambuliaji.blogsport.com
FRIKIKI ya Dakika ya 90 ya Lionel Messi imewanusuru Barcelona kipigo huko Estadio El Madrigal walipotoka 1-1 na Villareal kwenye Mechi ya La Liga iliyochezwa Jana.
 
Nicola Sansone aliwapeleka Villareal 1-0 mbele katika Dakika ya 50 kwa Shuti la chini alipopokea pasi toka kwa Alexandre Pato.
Baada ya hapo Messi alipiga Posti na Barca 'kunyimwa' Penati baada ya Bruno kunawa Mpira.
Huku Barca wakielekea kuchapwa, Messi alisawazisha kwa Frikiki murua.
Villareal, ambao wapo Nafasi ya 5, walimaliza Mechi hii Mtu 10 baada ya Jaume Costa kupewa Kadi ya Njano ya Pili na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu Dakika za Majeruhi.
Sare hiyo imewaacha Barca Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 1 nyuma ya Sevilla ambao wako Pointi 4 nyuma ya Vinara Real Madrid ambao wamecheza Mechi 1 pungufu kupita Timu zote.
VIKOSI:
VILLAREAL: Asenjo, Martínez, Musacchior, (González Soberón 87'), Ruiz, Costa Jordá, dos Santos, Trigueros Muñoz, Bruno, Soriano (Hernández Cascante 83'), Sansone, Pato(Castillejo Azuaga 76')
Akiba: N'Diaye, González Soberón, Fernández, Hernández Cascante, Castillejo Azuaga, Rukavina, Santos Borré
BARCELONA: Ter Stegen, Sergi, Piqué , Mascherano, Digne (Turan 71'), André Gomes(D Suárez 68'), Busquets, Iniesta, Neymar, L Suárez, Messi
Akiba: D Suárez, Turan, Rafinha, Alcácer, Alba, Umtiti, Masip
 Tokeo la picha la Ignacio Iglesias Villanueva
                                  Iglesias Villanueva
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment