TUZO YA FIFA YA MCHEZAJI BORA DUNIANI, JE RONALDO KUZOA TENA TUZO LEO?




Tokeo la picha la tuzo ya fifa image

CRISTIANO RONALDO, Mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani Ballon d'Or kwa Mwaka 2016 aliyopewa Mwezi uliopita Leo anapewa nafasi kubwa kuzoa Tuzo kama hiyo inayotolewa na FIFA. 

Leo huko Zurich, Uswisi, FIFA wanaendesha Hafla ya Tuzo za Ubora kwa Mwaka 2016.
Kabla Mwaka 2016, FIFA walishirikiana na Jarida la France Football kutoa Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani iliyoitwa FIFA Ballon d'Or lakini kuanzia Tuzo za 2016 washirika hao wametengana na kila Mtu kuenda kivyake.

Mwezi uliopita Ronaldo, Mchezaji wa Real Madrid kutoka Portugal, alimbwaga Lionel Messi, Mchezaji wa Barcelona kutoka Argentona, na kutwaa Ballon d'Or kwa mara ya 4 huku akiwa ameitwaa mara 5. 
 
 Safari hii Wawili hao watachuana na Antoine Griezmann kutoka Atletico Madrid na France kugombea FIFA Tuzo ya Mchezaji Bora kwa Mwaka 2016.
 
Sambamba na Tuzo hiyo pia Tuzo kadhaa zikigombewa ikiwemo.ile ya Kocha Bora Duniani kwa Mwaka 2016 na Wagombea wake ni Claudio Ranieri, alieiongoza Leicester City kutwaa Ubingwa wa EPL, Ligi Kuu England, Fernando Santos wa Portugal kwa kuiongoza Nchi hiyo kutwaa EURO 2016 na Zinedine Zidane, alieipa Real Madrid UEFA Championz Ligi.

Tuzo nyingine ni za Kinamama Mchezaji Bora Duniani, Tuzo ya Puskas kwa Goli Bora na Timu Bora ya Mwaka.

*************************************************
 
JINSI YA KUPATA WASHINDI KWA KUTUMIA KURA.
  • Washindi wa Tuzo hizi watapatikana kwa Kura:
  • Asilimia 50 ni ile ya Makepteni na Makocha wa Timu za Taifa za Nchi Wanachama FIFA
  • Asilimia 25 ya Kura itatoka kwa Kura za Mtandaoni za Mashabiki
  • Asilimia 25 ni Kura za Wawakilishi 200 wa Wanahabari kutoka Mabara yote 6 Duniani.

***********************************************************
Wagombea Watatu wa Goli Bora la Mwaka ni Marlone (Brazil/Corinthians), Daniuska Rodriguez (Venezuela/Venezuela Timu ya Taifa ya Wanawake U-17) na Mohd Faiz Subri (Malaysia/Penang). 
 
Kwa apande wa Kinamama Wagombea ni Jill Ellis (USA/Timu ya Taifa ya USA), Silvia Neid (Germany/Timu ya Taifa ya Germany) na Pia Sundhage (Sweden/Timu ya Taifa ya Sweden).

LISTI YA WACHEZAJI 55 WAGOMBEA WA KIKOSI BORA:
 
Goalkeepers MAKIPA
(5): Claudio Bravo (Chile/FC Barcelona/Manchester City), Gianluigi Buffon (Italy/Juventus), 
David de Gea (Spain/Manchester United), 
Keylor Navas (Costa Rica/Real Madrid) na 
Manuel Neuer (Germany/FC Bayern Munich).

MABEKI
(20): David Alaba (Austria/FC Bayern Munich), 
Jordi Alba (Spain/FC Barcelona),
Serge Aurier (CĂ´te d’Ivoire/Paris Saint-Germain), 
HĂ©ctor Bellerìn (Spain/Arsenal), 
JĂ©rĂ´me Boateng (Germany/FC Bayern Munich), 
Leonardo Bonucci (Italy/Juventus), 
Daniel Carvajal (Spain/Real Madrid), 
Giorgio Chiellini (Italy/Juventus), 
Dani Alves (Brazil/FC Barcelona/Juventus), 
David Luiz (Brazil/Paris Saint-Germain/Chelsea), 
Diego Godín (Uruguay/Atlético Madrid),
Mats Hummels (Germany/Borussia Dortmund/FC Bayern Munich), 
Philipp Lahm (Germany/FC Bayern Munich), 
Marcelo (Brazil/Real Madrid), 
Javier Mascherano (Argentina/FC Barcelona), 
Pepe (Portugal/Real Madrid), 
Gerard Piqué (Spain/FC Barcelona),
Sergio Ramos (Spain/Real Madrid), 
Thiago Silva (Brazil/Paris Saint-Germain) na
Raphaël Varane (France/Real Madrid).

VIUNGO
(15): Xabi Alonso (Spain/FC Bayern Munich), 
Sergio Busquets (Spain/FC Barcelona), 
Kevin De Bruyne (Belgium/Manchester City), 
Eden Hazard (Belgium/Chelsea), 
AndrĂ©s Iniesta (Spain/FC Barcelona), 
N’Golo KantĂ© (France/Leicester City/Chelsea) 
Toni Kroos (Germany/Real Madrid), 
Luka Modrić (Croatia/Real Madrid), 
Mesut Ă–zil (Germany/Arsenal), 
Dimitri Payet (France/West Ham United), 
Paul Pogba (France/Juventus/Manchester United), 
Ivan Rakitić (Croatia/FC Barcelona), 
David Silva (Spain/Manchester City), 
Marco Verratti (Italy/Paris Saint-Germain) na 
Arturo Vidal (Chile/FC Bayern Munich).
 
MASTRAIKA
 
(15): Sergio AgĂĽero (Argentina/Manchester City), 
Gareth Bale (Wales/Real Madrid), 
Karim Benzema (France/Real Madrid), 
Cristiano Ronaldo (Portugal/Real Madrid), 
Paulo Dybala (Argentina/Juventus), 
Antoine Griezmann (France/AtlĂ©tico Madrid), 
Gonzalo HiguaĂ­n (Argentina/Napoli/Juventus), 
Zlatan Ibrahimović (Sweden/Paris Saint Germain/Manchester United), 
Robert Lewandowski (Poland/FC Bayern Munich), 
Lionel Messi (Argentina/FC Barcelona), 
Thomas MĂĽller (Germany/FC Bayern Munich), 
Neymar (Brazil/FC Barcelona), 
Alexis Sánchez (Chile/Arsenal), 
Luis Suárez (Uruguay/FC Barcelona) na 
Jamie Vardy (England/Leicester City). 
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment