Kiungo mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Al Ahly na Misri, Mohamed
Aboutrika ameongezwa kwenye orodha ya magaidi nchini Misri kufuatia
kutuhumiwa kuwa na uhusiano na kikundi cha Muslim Brotherhood
kilichopigwa marufuku.
Aboutrika anatuhumiwa kukifadhili kikundi cha Brotherhood
kinachotafsiriwa kama kundi la kigaidi nchini Misri. Katika uchaguzi wa
mwaka 2012, Aboutrika alimpendekeza mgombea wa Brotherhood, Mohamed
Morsi ambaye alishinda urais na kudumu kwa kipindi cha mwaka mmoja
kabla ya kung’olewa madarakani na kuorodheshwa kwenye orodha ya magaidi
nchini humo.
Aboutrika pia amekuwa akiunga mkono nchi ya Palestina na kuvaa fulana
za kuwaunga mkono raia wa nchi hio katika vuguvugu dhidi ya Israel.
Wakili wa Aboutrika, Mohamed Osman amesema Aboutrika ameorodheshwa
kama gaidi licha ya kutofikishwa mahakamani wala kujulishwa kutuhumiwa.
” Tutakata rufaa kupinga haya maamuzi,” Amenukuliwa Osman huku Aboutrika mwenyewe akikana tuhuma hizo.
0 Maoni:
Post a Comment