Manchester United wameafiki dili ya kumuuza Memphis Depay kwa Klabu ya France Lyon.
Inaaminika Ada ya Uhamisho ni Pauni Milioni 16 na kupanda hadi
Pauni Milioni 21.7 ikitegemea vigezo kadhaa vikiwemo Lyon kufuzu kucheza
UEFA CHAMPIONZ LIGI na Depay kuongezewa Mkataba.
Pia kwenye Mkataba wa Mauzo wa Mchezaji huyo vipo Vipengeli
vinavyoruhusu Man United kumnunua tena na pia kuhusishwa akiuzwa kwa Klabu
nyingine.

Depay, mwenye Miaka 22 na ambae huichezea Timu ya Taifa ya
Netherlands, amefunga Bao 7 kwa Man United katika Mechi zake 53
alizocheza tangu ajiunge kutoka PSV Eindhoven Mei 2015 kwa Dau la Pauni
Milioni 25.
Msimu huu, Depay ameichezea Man United Mechi 8 tu lakini tangu Oktoba amecheza Dakika 8 tu.
Katika kipindi hiki cha Dirisha la Uhamisho la Januari, Depay
amekuwa Mchezaji wa Pili kuuzwa na Man United na mwingine ni Morgan
Schneiderlin alieuzwa kwa Everton Januari 12 kwa Ada ya Pauni Milioni
24.
0 Maoni:
Post a Comment