REAL MADRID Jana wakiwa kwao Santiago Bernabeu wamepokea kipigo
chao cha pili mfululizo baada ya kufungwa 2-1 na Celta Vigo katika Mechi ya
Kwanza ya Robo Fainali za Copa del Rey, Kombe la Mfalme wa Spain.
Real walikuwa kwenye mbio za Mechi 40 za kutofungwa lakini Wikiendi
iliyopita zikamalizwa walipochapwa 2-1 na Sevilla kwenye La Liga.
Kifungo cha Jana ni mara ya kwanza kwa Real kuchapwa Mechi 2 mfululizo tangu Novemba 2015.
Jana Celta Vigo walifunga Bao lao la Kwanza Dakika ya 64 kupitia
Iago Aspas aliewahi kuichezea Liverpool na Marcelo kusawazisha kwa
bunduki kali Dakika ya 69.

Dakika 1 baadae Celta Vigo wakafunga Bao la ushindi kupitia Castro Otto.
Timu hizi zitarudiana huko Galicia Jumatano ijayo na Mshindi kutinga Nusu Fainali.
0 Maoni:
Post a Comment