BAO
za Suarez, Neymar na Messi zimewapeleka Mabingwa Watetezi FC Barcelona
Robo Fainali ya Copa del Rey, Kombe la Mfalme wa Spain, walipoifunga
Athletic Bilbao 3-1 huko Nou Camp hapo Jana.
Wakiwa
wamefungwa 2-1 katika Mechi ya Kwanza, Barca walitangulia kufunga
Dakika ya 36 kwa Bao la Luis Suarez likiwa Bao lake la 100 katika Mechi
120 za Barca.
Neymar
aliongeza Bao la Pili Dakika ya 47 na Bilbao kupiga Bao lao moja Dakika
ya 51 kupitia Saborit na kufanya Gemu iwe Sare 3-3 kwa Mechi 2 lakini
Messi akapiga Bao la 3 Dakika ya 70 na kuwapa Barca ushindi wa 3-1 na
4-3 kwa Mechi Mbili.
0 Maoni:
Post a Comment