LIVERPOOL YAANGUKIA PUA EFL

 
Southampton imeifunga Liverpool 1-0 huko Saint Mary hapo Jana katika Mechi yao ya Kwanza ya Nusu Fainali ya EFL CUP, ambalo ndio Kombe la Ligi huko England.
 
Juzi, kwenye Mechi nyingine ya Kwanza ya Nusu Fainali nyingine iliyochezwa Old Trafford, Manchester United iliichapa Hull City Bao 2-0 kwa Bao za Juan Mata na Marouane Fellaini.

Bao la ushindi la Southampton, ambao ni maarufu kama ‘Watakatifu’, hapo Jana lilifungwa na Nathan Redmond baada kupokea Pasi ya Jay Rodriguez katika Dakika ya 20.

Southampton wangeweza kupata Bao nyingi kama si ushujaa wa Kipa wa Liverpool Loris Karius alieokoa Michomo mingi na hasa mara 2 kufuta kwenye chaki ya Goli Mipira ya Nathan Redmond.
 

Nusu Fainali hizi huchezwa kwa Mikondo Miwili ya Nyumbani na Ugenini na hivyo Marudiano ya Mechi hizi yatakuwa hapo Januari 25 na 26 huko Anfield na KCOM Stadium.

EFL CUP
Nusu Fainali
MARUDIANO

++Saa za Bongo++
Kwenye Mabano Mabao Mechi ya Kwanza

Jumatano Januari 25
2300 Liverpool v Southampton [0-1]

Alhamisi Januari 26
2245 Hull City v Manchester United [0-2]
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment