ULE
Uhamisho wa Mbrazil Gabriel Jesus kwenda Manchester City bado haujapata
Saini ya mwisho ingawa Meneja Pep Guardiola anatarajia utakamilika
kabla hawajasafiri kwenda Liverpool Jumapili kucheza na Everton huko
Goodison Park kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England.
City
walishafikia makubaliano na Klabu ya Brazil Palmeiras tangu Mwezi Julai
Mwaka Jana kumnunua Kinda huyo wa Brazil mwenye Miaka 19 kwa Dau la
Pauni Milioni 27 na pia kukubali Mchezaji huyo abakie Palmeiras hadi
Msimu wa Brazil utakapoisha Mwezi Desemba.
Jesus
amekuwa Kambini na City kwa Wiki 2 sasa lakini ukiritimba umekwamisha
Uhamisho wake kukamilika rasmi na hivyo kusitisha kuichezea rasmi City.
Kinda
huyo ndio kwanza amechomoza kwenye Soka la Dunia akiwa na Msimu wa Pili
tu na Palmeiras lakini akaiongoza Klabu hiyo kutwaa Ubingwa wa Taifa
Mwezi Novemba baada ya kutwaa Medali ya Dhahabu akiichezea Brazil kwenye
Michezo ya Olimpiki, RIO 2016, Mwezi Julai.
Jesus
alianza kukichezea Kikosi cha Kwanza cha Timu ya Taifa ya Brazil Mwezi
Septemba Mwaka Jana na kufunga Bao 4 katika Mechi zake 6.
0 Maoni:
Post a Comment