
Baada
ya Yanga kufanya vibaya kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi
iliyomalizika hivi karibuni, Katibu wa Baraza la Wazee la Yanga, Ibrahim
Akilimali, ameuomba uongozi wa klabu hiyo kuliangalia kwa umakini suala
la kutofautiana kwa kocha mkuu, Mzambia, George Lwandamina na
Mkurugenzi wa Benchi la Ufundi, Mholanzi, Hans van Der Pluijm.
Hivi
karibuni, baada ya Yanga kuondoshwa na Simba hatua ya nusu fainali ya
Kombe la Mapinduzi, kuliibuka madai kwamba Pluijm amekuwa hana uhusiano
mzuri na kocha huyo raia wa Zambia hali ambayo ilipelekea Mholanzi huyo
kutakiwa kuondoka.
Akilimali
alisema kuwa uongozi wa juu wa klabu hiyo unapaswa kuliangalia kwa
umakini suala la makocha hao kwani linaweza kuwa sababu kubwa ya timu
kufanya vibaya.
"Kiukweli
hili suala la Lwandamina na Pluijm uongozi niombe uliangalie kwa
umakini mkubwa kwa sababu nijuavyo ni kwamba mafahari wawili hawawezi
kukaa zizi moja na hilo lipo wazi, sasa lazima zichukuliwe hatua kwa
manufaa ya timu.
"Unajua
wakati Pluijm alipokuwa kocha wa Yanga hakuwa na rekodi mbaya kabla ya
kupewa cheo kingine, sasa kibinadamu lazima awe na kinyongo na mwenzake,
unadhani atakuwa anatoa ushauri sawasawa, ukiangalia hata wachezaji
bado wanampenda, niwaombe sana viongozi wangu kuliangalia hili ili
tuweze kutetea ubingwa wetu na siyo tufanye malumbano, tunataka
turudishe umoja wetu kama zamani," alisema Akilimali.
0 Maoni:
Post a Comment