Baada
ya mwanariadha Mtanzania, Alphonce Simbu kufanikiwa kuibuka mshindi wa
mbio za Mumbai Marathon, wikiendi iliyopita, Chama cha Riadha Tanzania
(RT), sasa kimempa jukumu la kwenda London kuchukua medali nyingine.
Simbu
ambaye kwenye mbio hizo alifanikiwa kushika nafasi ya kwanza na
kuondoka na medali pamoja na kitita cha dola 67,000 ambazo ni sawa na Sh
milioni 147 za Kitanzania, Agosti mwaka huu anatarajiwa kushiriki mbio
za World Athletic Championship zitakazofanyika London, England.
Juzi
Jumatatu, mwanariadha huyo alitua nchini kwenye Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na siku yoyote anatarajia kutua jijini
Dar ambapo ataandaliwa tafrija ya kupongezwa na wadhamini wake, Kampuni
ya DStv.
Katibu
Mkuu wa RT, Wilhelm Gidabuday, ameliambia Championi Jumatano kuwa:
“Fedha alizopata zimegawanyika sehemu tatu na kufikia hizo dola 67,000,
zawadi za mshindi wa kwanza ni dola 42,000, lakini kutokana na kufanya
kwake vizuri kwenye Olimpiki alipata mwaliko maalum ambao ulikuwa na
kipengele kwamba akishinda au akishindwa lazima apewe dola 15,000 na
wastani mzuri wa kukimbia akapata bonasi ya dola 10,000.
“Kilichobaki
sasa tunataka aende London kwenye mashindano ya World Athletic
Championship na kurudi na medali, tukipata medali huko ni heshima kubwa
kwani haya ni ya pili kwa ukubwa ukiondoa Olimpiki.”
0 Maoni:
Post a Comment