Uongozi
wa Azam FC umetamka kwamba utafanya kila linalowezekana kuendeleza
makali yao waliyoyaonyesha katika Kombe la Mapinduzi kwenye michezo yao
ya ligi wakianza kufanya hivyo leo dhidi ya Mbeya City.
Kikosi
hicho cha Azam kinachofundishwa na Mromania, Aristica Cioaba
kilifanikiwa kutwaa ubingwa wa Mapinduzi visiwani Zanzibar kwa kuwafunga
Simba bao 1-0, ambapo leo Jumatano watawavaa Mbeya City katika Uwanja
wa Azam Complex, Dar.
Msemaji
wa timu hiyo, Jaffar Idd amesema kuwa tayari wamejipanga kuona
wanaondoa matokeo mabaya waliyokuwa nayo kwenye mechi zao za nyuma kwa
kuhakikisha wanacheza kwa kiwango cha juu kama walivyofanya Zanzibar.
“Tumepania
kwamba matokeo mabaya tuliyokuwa nayo kabla kwenye mechi zetu za ligi
yanabaki historia kwa kujipanga na kuibuka upya huku tukitaka kumaliza
mechi zetu tukipata matokeo mazuri.
“Hilo
tumelifanyia kazi na tutaanza kulionyesha leo tutakapowavaa Mbeya City
ambapo timu ina morali kubwa ya kuona kwamba inapata ushindi kwa ajili
ya kurudi kwenye mstari wake baada ya kupepesuka kwenye mechi za awali,”
alisema Idd.
0 Maoni:
Post a Comment