JANA Nahodha wa Real Madrid ambao ni Vinara wa La Liga Sergio Ramos alifunga
Bao 2 wakati Timu yake ikiichapa 2-1 Malaga huko Santiago Bernabeu
kwenye Mechi ya Ligi ambayo Nyota wa Real Cristiano Ronaldo akizomewa na
baadhi ya Mashabiki wa Timu hiyo.
Baada ya Mechi 18 kwa kila Timu Real wanaongoza La Liga wakiwa na
Pointi 43 wakifuatiwa na Sevilla wenye 39, Barcelona 38 na kisha Atletico
Madrid wenye 34.
Jana Ramos alifunga Bao la Kwanza Dakika ya 35 kwa Kichwa kufuatia
Kona ya Toni Kroos na kisha kupiga la pili Dakika ya 43 huku Malaga
wakifunga Bao lao moja Dakika ya 63 kupitia Juanpi Anor.
Kwenye Mechi hiyo Ronaldo alikosa nafasi kadhaa zilizookolewa na
Kipa Kameni na moja kupiga Posti kitu ambacho kiliwachukiza Mashabiki
ambao baadhi yao walimzomea.
Kitu hicho kilimsikitisha Meneja wa Real Zinedine Zidane ambae aliwaasa Mashabiki hao kuwapa moyo Wachezaji.
Leo Timu za Pili na za 3, Sevilla na Barca, zipo Ugenini kucheza Mechi zao za La Liga.
0 Maoni:
Post a Comment