WAKATI Asamoah Gyan akiifungia Ghana Bao pekee walipoifunga Mali
1-0 huko Gabon katika Mechi ya Pili ya Kundi D la AFCON 2017, Egypt,
katika Mechi nyingine ya Kundi D, waliifunga Uganda 1-0 na kuwatupa nje
Uganda katika Mashindano hayo.
Mapema Jana huko Port-Gentil, Gyan alifunga Bao pekee na kuifanya
Ghana wawe Nchi ya Pili kutinga Robo Fainali baada ya Juzi Senegal nao
kusonga wakibakisha Mechi 1 katika Makundi yao.
Katika Mechi ya Pili ya Kundi D, Bao la Dakika ya 89 la Mchezaji
alieanzia Benchi Abdallah El Said liliipa ushindi Egypt wa 1-0 na kuitupa
Uganda nje ya Nashindano huku wakibakisha Mechi 1.
Katika Mechi ya mwisho, Ghana watacheza na Egypt hapa Jumatano na Egypt wanahitaji Sare tu ili kufuzu.
Siku hiyohiyo Mali watahitaji kuifunga Uganda Siku hiyo ya Jumatano huku wakiomba Egypt ifungwe ili wao wafuzu
Leo Jumapili zipo Mechi za mwisho za Kundi A huko Libreville ambapo
Wenyeji Gabon watalazimika kuifunga Cameroon ili kufuzu na Sare
itawaacha waombe matokeo mema kwao katika Mechi nyingine ya Kundi hilo
kati ya Burkina Faso na Guinea-Bissau.
Jana Rais wa Gabon Ali Bongo aliwatembelea Wachezaji wa Nchi hiyo ili kuwapa morali
0 Maoni:
Post a Comment