MAN CITY na Tottenham Hotspur Jana zilitoka Sare 2-2 huko Etihad Jijini Manchester katika Mechi ya EPL, Ligi Kuu England.
City
walitangulia kufunga katika Dakika za 49 na 54 kupitia Leroy Sane na
Kevin De Bruyne na Spurs kusawazisha Dakika za 58 na 77 kwa Bao za Dele
Alli na Son Heung-min.
Mchezaji Mpya wa City kutoka Brazil, aliingizwa mwishoni kutoka Benchi na kufunga lakini Bao hilo lilikataliwa kwa kuwa Ofsaidi.
Matokeo hayo yamewaacha City Nafasi ya 5 huku Spurs wapo Nafasi ya Pili.
Mapema hiyo hiyo Jana huko Anfield, Liverpool walichapwa 3-2 na Swansea City katika Mechi nyingine ya EPL.
Bao
za Liverpool zilipachikwa Dakika za 56 na 69 na Firmino wakati Swansea
walifunga Dakika za 48 na 52 kwa Bao za Llorente na 74 la Gylfi
Sigurdsson.
0 Maoni:
Post a Comment