Wayne Rooney amekuwa Mfungaji Bora katika Historia ya Manchester United baada ya Frikiki yake ya Dakika za Majeruhi kuwapa Sare ya 1-1 walipocheza na Stoke City katika Mechi ya EPL, Ligi Kuu England huko Bet 365 Stadium.
Stoke walitangulia kufunga katika Dakika ya 19 kwa Bao la kujifunga mwenyewe Juan Mata alietumbukiza Mpira wavuni kutokana na Krosi ya Erik Pieters.
Rooney, alieingizwa kutoka Benchi katika Dakika ya 67 kumbadili Mata, alipiga Frikiki ya Dakika ya 94 na kufunga Bao lake la 250 kwa Man United alimzidi aliekuwa akishikilia Rekodi Sir Bobby Charlton ya Bao 249.
Bao hilo limedumisha Rekodi ya Man United ya kutofungwa katika Mechi 17 lakini limewaweka wakiwa Pointi 3 kutoka Timu ya 4 Arsenal na wapo Pointi 11 kutoka kwa Vinara Chelsea.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Ratiba Ligi Kuu England
Saa za Bongo
Jumapili Januari 22
1500 Southampton v Leicester City
1715 Arsenal v Burnley
1930 Chelsea v Hull City
0 Maoni:
Post a Comment