Diego Costa anataka kuendelea
kusalia Chelsea na ni miongoni mwa wachezaji walio tayari kucheza mechi
ya Ligi Kuu ya Engand dhidi ya Hull Jumapili, meneja Antonio Conte
amesema.
Costa, 28, aliachwa nje ya kikosi kilichoshinda mechi ya
wikendi iliyopita dhidi ya Leicester baada ya kuzozana na mmoja wa
wakufunzi kuhusu hali yake.
Hayo yalijiri huku kukiwa na uvumi kwamba alikuwa anatafutwa na klabu za Uchina.
Chelsea
walisema aliachwa nje kutokana na maumivu ya mgongo, na kwamba alikuwa
amefanya mazoezi pekee kwa siku mbili kama sehemu ya juhudi za kumsaidia
kupata nafuu.
"Ana furaha kuendelea kutuchezea. Sioni tatizo lolote, alisema Conte.
"Nimesikia
uvumi mwingi kumhusu Diego, la muhimu sasa ni kwamba alifanya mazoezi
nasi wiki hii, hana maumivu mgongoni na anaweza kucheza.
"Yeye ni mchezaji muhimu sana kwetu na sote twajua hilo. Akiwa katika hali nzuri, amekuwa akituchezea."
Costa atapata mkataba mpya? Begovic ataondoka?
Siku
chache kabla ya Chelsea kuilaza Leicester 3-0 , Costa alikuwa
amehusishwa na kuhamia klabu moja ya China kwa £30m kila mwaka.
Mmiliki
wa klabu ya Ligi Kuu ya China Tianjin Quanjian alisema alitaka kumnunua
Costa lakini sheria mpya kuhusu kuchezesha wachezaji wa nje ya nchi
zikamzuia.
kiungomshambuliaji imefahamu kwamba Chelsea hawataki kumuuza Costa,
ambaye ndiye mfungaji mabao bora wao msimu huu. Mkataba wake ni wa hadi
Juni 2019.
Conte hata hivyo hakusema iwapo Costa ataanza mechi hiyo ya Jumapili dhidi ya Hull.
KUhusu mkataba mpya, alisema kwa sasa ni vyema kufikiria kuhusu ya sasa.
Hayo yakijiri, Conte amesema klabu hiyo inatathmini ofa kutoka kwa klabu zinazomtaka kipa Asmir Begovic.
Hata
hivyo, alisema kipa huyo wa Bosnia, 29, ambaye amehusishwa na kuhamia
Bournemouth, ni mchezaji "muhimu sana katika kikosi (cha Chelsea)".
0 Maoni:
Post a Comment