West Ham imemsajili nahodha wa Southampton Jose Fonte kwa kima cha pauni milioni 8 kwa mkataba wa miaka miwili unusu.
Fonte
raia wa Ureno mwenye umri wa miaka 33 ambaye aliichezea Southampton kwa
miaka saba, aliomba kuihamia West Ham ikiwa imesalia miezi 18 kabla ya
mkataba wake kumalizika.
Mkurugenzi wa Southampton Les Reed anasema kuwa Fonte alikuwa na fursa ya kusaini mkataba bora lakini akaomba kuondoka.
Fonte amesema kuwa meneja wa West Ham Slaven Bilic alichangia pakubwa kumshawishi kuichagua West Ham.
0 Maoni:
Post a Comment